HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Rais Kenyatta,IEBC wataka kesi ya Omtata itupiliwe mbali

Rais Uhuru Kenyatta na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC sasa wameitaka mahakama ya IEBC kufutilia mbali kesi iliyowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtata, wakisema imepitwa na wakati na matukio mahakamani.
Kwenye kauli yao waliyowasilisha mahakamani kupitia kwa mawakili wao, IEBC na Rais Kenyatta wamesema mahakama ya upeo kwa sasa haina mamlaka ya kusikiza kesi hiyo kwani tayari majaji wametoa ratiba ya jinsi kesi hiyo itaendeshwa.
Haya yanajiri huku Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu akitarajiwa kuteua jopo la majaji wa kuisikiliza kesi hiyo kama anavyotuarifu.

Show More

Related Articles