HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wapangaji waagizwa kuhama kufuatia dalili za kuporomoka

Wapangaji wa nyumba moja mtaani Kasarani hapa jijini Nairobi, wamelazimika kuhama, baada ya  nyumba hiyo kuonyesha dalili za kuporomoka .
Kulingana na mmoja wa wapangaji, jumba hilo lilianza kudhihirisha nyufa , huku kuta zake zikionyesha dalili za kuporomoka.
Inadaiwa kuwa nyumba hiyo ilianza kuonyesha dalili hizo baada ya jengo linalopakana nayo kulalia nyumba hiyo.

Show More

Related Articles