HabariMilele FmSwahili

Jamaa anayedaiwa kushuhudia ajali ya Kabati na ziwa Nakuru kukesha korokoroni

Jamaa anayedaiwa kuwa shahidi wa ajali mbili katika maeneo Kabati huko Muranga na ziwa Nakuru atakesha korokoroni leo. Dennis Ngengi alikamatwa hujo juja baada ya kudai kunukuliwa katika vyombo vya habari akishuhudia kuhusu ajali iliyopelekea kifo cha gavana wa Nyeri Dkt Wahome Gakuru ambapo pia alijitambua awali katika ziwa Nakuru alinukuliwa pia akizungumzia ajali ya helikopta iliyosababisha vifo vya watu watano na kudai kuwa rafikiye rubani Apollo Malowa. Mkuu wa jinai Ndegwa Muhoro amedhibitisha kuzuiliwa kwake ili kuwapa majasusi muda wa kumchunguza.

Show More

Related Articles