HabariMilele FmSwahili

Bunge la Vihiga lapitisha hoja ya kuunda bunge la mwananchi lililowasilishwa na NASA

Bunge la kaunti ya Vihiga limepitisha hoja ya kuunda  bunge la mwananchi iliyowasilishwa na  mrengo wa NASA. Akiwasilisha hoja za kiongozi wa wengi Wycliff Masini alisema baadhi ya maswala yaliyowasukuma kuleta mswada huo bungeni.
Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi wa NASA akiwemo Seneta wa Siaya James Orengo, Seneta wa Kakamega  Cleofas Malala, mbunge wa Mathare Anthony Oluoch na mbunge mteule Godfrey Osotsi, na mwakilishi wa kina mama wa kaunti ya Homabay Gladys Wanga. Naye aliyekuwa seneta wa kaunti ya Kakamega Bonny Khalwale ameelezea imani kuwa hoja hiyo itapitishwa katika mabunge ya kaunti 24 ili kufanikisha azma ya NASA.

Show More

Related Articles