Pilipili FmPilipili FM News

Kinamama wajawazito Walalamikia Kudhalilishwa na Wataalam katika Hospitali ya Moi Mjini Voi

Kinamama wajawazito wanaotafuta huduma za afya katika hospitali ya Moi mjini Voi, wanalalamikia kudhalilishwa na wataalam katika hospitali hiyo pale wanapoenda kutafuta matibabu.

Wengi wao wanasema hushinda siku mzima bila kuhudumiwa katika hospitali hiyo licha ya wao kufika mapema, huku wengine wakidai kumaliza juma moja bila kushughulikiwa.

Wamemtaka gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja pamoja na wizara ya afya kuingilia kati suala hilo kuwachunguza na kuwachukulia hatua maafisa wa afya wanaozembea kazini.

Show More

Related Articles