HabariMilele FmSwahili

Mahakama kusikiza kesi iliyowasilishwa na mwanaharakati Omtata kufutilia mbali uchaguzi wa Oktoba 26 leo

Mahakama ya upeo leo itaskiza kesi iliyowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtata akitaka kufutilia mbali uchaguzi wa Oktoba 26. Kwenye kesi hiyo Omtata anasema uchaguzi huo haukuzingatia sheria kwani wagombea hawakupitia mchujo. Hata hivyo IEBC ikijibu kwenye kesi hiyo imetaka mahakama hiyo kutupilia mbali kesi yake Omtata. Katika hati kiapo, IEBC kupitia mwenyekiti Wafula Chebukati inasema marudio ya uchaguzi wa urais yaliafikia vigezo vyote vya sheria. IEBC pia inasema Omtata aliwasilisha kesi hiyo kabla ya kutangazwa kwa rais Uhuru Kenyatta kama mshindi na hivyo haiambatani na sheria. Ameongeza mahakama ya juu haina mamlaka ya kuskiza kesi hiyo. Omtata amepzilia mbali suala hilo akisema yuko tayari kwa kesi hiyo.

Show More

Related Articles