People Daily

Wajenzi Bandia Nchini Waonywa

Katibu katika idara ya kitaifa ya ukaguzi na ujenzi Moses Nyakironga ametoa onyo kali kwa wajenzi bandia nchini akisema watakabiliwa kisheria.
Akizungumza kwenye kikao na wadau katika sekta hiyo hapa Mombasa, Nyakironga ameilaumu idara ya mahakama kwa kujikokota katika kushughulikia kesi zinazohusiana na kuporomoka kwa majumba hafifu nchini.

Naye rais wa chama cha wajenzi Emma Miloyo amesema wanatazamia kuimarisha ujenzi wa barabara, majumba ya bei nafuu na kupanua nafasi za umma ili kufanikisha maendeleo.

Show More

Related Articles