HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Wasiotambulika : Patrick anayewanywesha wanyama pori atambulika ulimwenguni

Unakumbuka jamaa mmoja kutoka Voi ambaye alikuwa amejitolea kusafirisha maji kwenda mwituni Tsavo West akiwapelekea wanyama pori waliokuwa wakiiteseka kwa ukame?
Ni takriban mwaka mmoja hivi tangu ripota wetu Dennis Matara kumwangazia Patrick Mwalua kwenye makala ya Wasiotambulika na kufuatia taarifa hiyo, Patrick alipata umaarufu duniani na kupata wafadhili, na hivi sasa, Patrick ameweza kujinunulia lori la kubebea maji ya wanyama pori na pia kununua vifaa kadha vya sola na mabomba ya kusukuma maji porini, yote kwa ajili ya kumaliza kiu ya wanyama pori Tsavo.
Dennis Matara tena na taarifa yake kutoka mbuga ya wanyama pori ya Tsavo West

Show More

Related Articles