HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Uamuzi wa Mahakama ya Upeo kuamua hatima yake na makamishna

Hatma ya mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC Wafula Chebukati na makamishna wenzake itajulikana tarehe ishirini mwezi huu, ikiwa ni siku ambayo mahakama ya upeo itatoa uamuzi wake kuhusiana na kesi za marudio ya uchaguzi wa urais.
Iwapo mahakama hiyo itaamua kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo, basi huenda utendakazi wa Chebukati na makamishna wake ukatiliwa shaka na yamkini kutimuliwa kutoka afisi, kwani hii itakuwa ni mara ya pili kitumbua chao kuingia mchanga.
Hata hivyo wadadisi wa masuala ya uchaguzi wanasema iwapo mahakama itashikilia ushindi wa rais Kenyatta, basi Chebukati atakuwa amejiondolea lawama dhidi yake na makamishana wake kama anavyotuarifu Kiama Kariuki.

Show More

Related Articles