HabariMilele FmSwahili

Rais azuru nyumbani kwa mwendazake Gavana Wahome kufajiri familia yake

Rais Uhuru Kenyatta amezuru nyumbani kwa mwendazake gavana wa Nyeri dr Wahome Gakuru mtaani Runda Nairobi. Rais ametumia fursa hiyi kufariji familia ya Gakuru na kutoa hakikisho serikali itakua pamoja nao wakati huu mgumu. Hayo yanajiri huku, maafisa wa polisi wanaochunguza kifo cha Gakuru wakisema watatumia ushahidi wa maafisa wa wizara ya uchukuzi,wale wa kampuni ya kutengeza magari ya DT Dobie na wetengenezaji magurudumu ya Pirelli. Tayari uchunguzi huo unaendelea watu kadhaa wakiohojiwa.

Show More

Related Articles