HabariMilele FmSwahili

Kesi ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa gavana wa Garissa Nadhif Jama yatupiliwa mbali

Kesi ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa gavana wa Garisa Nadhif Jama imetupiliwa mbali. Tume ya kukabiliana na ufisadi EACC ilimshitaki Jama na washukiwa wengine sita kutoka idara ya ununuzi wa iliyokuwa serikali yake kwa madai ya kukiuka sheria katika kukodisha magari saba ya kubeba wagonjwa kutoka shirika la msalaba mwekundu. Hata hivyo hakimu mkuu wa mahakama ya Garisa Cosmas Maundu ameamua kuwa mashahidi kwenye kesi hiyo walitoa maelezo ya kukanganya. Jama amepongeza uamuzi huo akisema madai dhidi yake hayakuwa na msingi.

Show More

Related Articles