HabariMilele FmSwahili

Twitter yawaruhusu wateja wake kutumia tarakimu 280 kuandika ujumbe

Twitter imetangaza kwamba imeanza kuwafungulia watu wanaoutumia mtandao huo wa kijamii uwezo wa kuandika ujumbe kwa kutumia tarakimu 280 badala ya 140. Kampuni hiyo ilikuwa imewawezesha baadhi ya watu kutumia tarakimu hizo lakini kwa majaribio tangu Septemba.

Watakaozuiwa pekee ni wale wanaoandika ujumbe kwa Kijapani, Kichina na Kikorea ambao wanaweza kuwasilisha maelezo zaidi kwa kutumia tarakimu chache. Wamesema majaribio yalifanikiwa. Mabadiliko hayo ni sehemu ya mpango wa Twitter kuwavutia watu zaidi.

Show More

Related Articles