HabariMilele FmSwahili

Wahadhiri wanaoandamana wakabiliwa na polisi katikati mwa jiji la Nairobi

Wahadhiri wanaoandamana wamekabiliwa na wakati mgumu baada ya polisi kujaribu kutatiza maandamano yao katikati mwa jiji la Nairobi. Hata hivyo wahadhiri hao wamefanikiwa kuwasilisha waraka wao kwa bunge  la kitaifa na kupokelewa na Wabunge Otiende Amollo na Wilson Sossion. Hata hivyo katibu wa UASU Constatine Wasonga anasema mgomo wao uliaonza  juma jana umekuwa na ufanisi katika vyuo vyote  31 vikuu nchini. Anapinga kutekelezwa kwa  mkataba wao katika awamu. Naye mwenyekiti wa UASU Muga Kolale anasema wizara ya fedha imekuwa ikishirikiana na ile ya elimu kulemaza juhudi za wahadhiri kupata haki. Wahadhiri hao ambao wameanza maandamano ya kila juma wanashinikiza nyongeza ya mshahara na marupuru ya nyumba.

Show More

Related Articles