HabariMilele FmSwahili

Uhuru aongoza mkutano wa jopo kazi la kuipa kaunti ya Nairobi sura mpya

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza mkutano wa jopo kazi la kuipa sura mpya kaunti ya Nairobi. Mpango huo unaoendeshwa na serikali kuu kwa ushirikiano na kaunti ya Nairobi unalenga kukwamua sekta muhimu za kiuchumi na kijamii na kuinua maisha ya wenyeji. Mkutano huo uliohudhuriwa na gavana Mike Sonko umeafikia kuwa katika mwezi mmoja ujao idara za ununuzi za serikali kuu na kaunti ziainishe mipangilio yao ili kuhakikisha kiasi kinachohitajika cha fedha kinatengewa mradi huo. Mradi huo utajumuisha kuboresha sekta za uchukuzi, makaazi na miradi ya kuwafaa vijana kina mama na watu wenye changamoto ya ulemavu.

Show More

Related Articles