HabariPilipili FmPilipili FM News

Mvua Ya Tataiza Shughli Za Usafiri LungaLunga

Wakaazi wa eneo la Ganda , lungalunga kaunti ya kwale wanalalamikia kuzorota kwa huduma za usafiri kufuatia ubovu wa barabara, hali ambayo wanasema imechangiwa na mvua kubwa iliyonyesha katika kaunti hiyo hivi majuzi.
Wanaishtumu serikali ya kaunti hiyo kwa kuchelewesha ukarabati wa barabara inayoelekea katika shule ya msingi ya GANDA.
Aidha wanadai kuwa mwanakandarasi anayeshughulikia barabara hiyo anaendesha zoezi hilo polepole, hali ambayo wameitaja kukwamisha shughuli nyingi muhimu eneo hilo.

Show More

Related Articles