HabariMilele FmSwahili

Kenya yaiandikia Tanzania kulalamikia hatua ya kuwauza ng’ombe walioingia nchini humo kimakosa

Serikali ya Kenya imeandikia Tanzania barua ya kulalamimikia hatua ya taifa hilo kuwauza ng’ombe na kuku wa wakenya walioingia nchini humo kimakosa. Waziri wa masuala ya kigeni Amina Mohammed anasema mbali na barua hiyo,waziri mwenza wa Leba Phillis Kandie ameelekea Tanzania kulalamikia hatua hiyo na kushinikiza haki kutendewa waathiriwa.
Yakijiri hayo,waziri Mohammed amepuzilia mbali shinikizo za baadhi ya wanasiasa wa Pwani kuanzisha mchakato w akujitenga. Amesisitiza Kenya ni taifa moja lililo na kaunti 47 kwa mujibu wa katiba hivyo hatua hiyo haitakubalika kamwe.

Show More

Related Articles