HabariMilele FmSwahili

Wabunge wa NASA waishutumu serikali kwa kufeli kutatua mgogoro kuhusu umiliki wa kisiwa cha Migingo

Wabunge wa NASA wameishutumu serikali ya Jubilee kwa kufeli kutatua mgogoro kuhusiana na umiliki wa kisiwa cha Migingo. Wakiongozwa na mwenyekiti wa ODM John Mbadi na mbunge Milly Odhiamo wabunge hao wanadai serikali imepuuza kilio cha wavuvi wa Kenya wanaoendelea kukamatwa na kuhangaishwa na askari kutoka Uganda. Wanadai wavuvi wawili wamekamatwa na kuzuiliwa bila sababu mwafaka
Wamemtaka inspekta jenerali Joseph Boinet kuhakikisha usalama unaimarishwa katika kisiwa hicho ili kuhakikisha haki za wavuvi hazikiukwi.

Show More

Related Articles