HabariMilele FmSwahili

Wahadhiri wa vyuo vikuu kuanza maandamano leo kushinikiza utekelezaji wa mkataba wao

Wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini wataanza maandamano leo kushinikiza serikali kutekeleza mkataba wao wa mwaka 2014-2017. Wahadhiri wanatarajiwa kukongamana katika uwanja wa chuo kikuu cha Nairobi ambako maandamano hayo yataanza. Aidha wameratibiwa kuelekea katika bunge la ofisi za wizara ya elimu kuwasilisha matakwa yao. Katibu Constatine Wesonga anasema watashiriki maandamano hayo kila jumatano hadi kilio chao kisikike

Show More

Related Articles