HabariMilele FmSwahili

Richard Onyonka ahifadhi kiti chake baada ya uchaguzi wa Kitutu Chache kusini

Richard Onyonka amehifadhi kiti chake baada ya kuwashinda wawaniaji wengine sita katika uchaguzi wa Kitutu Chache kusini uliofanyika jana. Onyonka aliyewania kwa tiketi ya Ford Kenya ameibuka mshindi kwa kura 10,122 akifuatiwa na Antony Kibagendi wa jubilee kwa kura 5,074. Samwel Omwando wa ODM amemaliza wa tatu kwa kura 4,324. Afisa msimamizi wa uchaguzi Hilda Yimbo amemtangaza Onyonka mshindi. Onyonka amewashukuru wapiga kura eneo hilo kwa kumchagua na kuahidi kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Show More

Related Articles