HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Gavana Wahome Gakuru alifariki kufuatia ajali eneo la Kabati

Wakenya wanazidi kuomboleza kifo cha gavana wa pili wa kaunti ya Nyeri , dkt Wahome Gakuru , aliyekumbana na mauti alfajiri ya leo , katika eneo la Kabati , kwenye barabara ya kutoka Nyeri kuelekea Nairobi.
Duru zinaashiria kuwa dereva wa gari la gavana alipoteza mwelekeo akijaribu kukwepa kumgomnga mwendeshaji bodaboda , na kugonga mabati yaliyoko kando ya barabara.
Mabati hayo yalipasua gari lake na kumuumiza vibaya .
Watu wengine wawili waliokuwa wakisafiri na gavana walijeruhiwa , lakini dereva wake hakujeruhiwa .
Frankline Macharia anasimulia.

Show More

Related Articles