HabariPilipili FmPilipili FM News

Watu Saba Wakamatwa Kwa Kutumia Mifuko ya Plastiki

Abiria wanaotupa mifuko ya plastiki nje ya magari ya usafiri watatozwa faini ya shilingi elfu tano.

Haya yamesemwa na mamlaka ya kusimamia mazingira NEMA ambayo imezindua ushirikiano na mamlaka ya usalama barabarani NTSA kufanikisha mipango hii.

Afisa mkuu wa NEMA kanda ya magharibi na kaskazini mwa bonde la ufa amesema watafuatilia kuhakikisha agizo hili linatekelezwa.

Tayari watu saba wamekamatwa na mamlaka hiyo na kufikishwa kortini kutokana na matumizi ya plastiki zilizopigwa marufuku.

 

Show More

Related Articles