HabariPilipili FmPilipili FM News

Baraza la Magavana la Omboleza Kifo cha Wahome Gakuru

Magavana kutoka kaunti mbali mbali wametuma risala za rambi rambi, kwa familia, marafiki na wenyeji wa kaunti ya Nyeri kufuatia kifo cha Gavana wa kaunti hiyo DKT Wahome Gakuru.
Wakiongozwa na mwenye kiti wa baraza la magavana josphat Nanok wamesema ni kisa cha kuhuzunisha ikizingatiwa kwamba Gakuru ni Gavana wa pili kufariki akiwa mamlakani katika kaunti hiyo ya Nyeri.
Aidha wamemtaja Gakuru kama mtu mnyenyekevu na mwenye bidii katika utendakazi wake.

Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonki, amekashifu sheria inayo ruhusu naibu wa gavana kuchukua hatamu za uongozi pindi tu Gavana anapofariki.

Show More

Related Articles