HabariMilele FmSwahili

Magavana wataka uchunguzi wa haraka kufanyika kubaini kilichosababisha ajali iliyomuua Gavana Wahome

Baraza la magavana linataka uchunguzi wa haraka kufanyikiwa kubaini kilichosababisha ajali ya barabara iliyogharimu maisha ya gavana wa Nyeri Dr Wahome Gakuru. Mwenyektii Josphat Nanok anasema licha ya kwamba wameelezwa ilikuwa ajali ya barabarani wanataka kufahamu zaidi kilichopelekea ajali hiyo. Yakiarifiwa hayo gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amependekeza mabadiliko kwenye kipengee cha 182 ibara ya 2 cha katiba kuhusu jinsi naibu gavana anafaa kuchukua hatamu za uongozi katika kisa cha gavana kufariki. Anasema shughuli hiyo haifakuwa mara moja Gakuru alikumbana na mauti yake baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani eneo la kabati kwenye barabara kuu ya Thika-Sagana. Wahome mwenye miaka 51, ni gavana wa pili wa Nyeri kufariki katika kipindi cha mwaka mmoja.

Show More

Related Articles