HabariPilipili FmPilipili FM News

Kampuni Ya Base Titanium Ya Dinda Kuwalipa Wakaazi Wa Vumbu

Usimamizi wa Kampuni Ya uchimbaji madini ya Base Titanium kaunti ya kwale unasema kampuni hiyo haitawalipa Ridhaa Wala Kuwahamisha Wakaazi Wa Kijiji Cha Vumbu Kama Inavyodaiwa , licha ya Wakaazi Wa Kijiji hicho kulalama kutokana na athari za vumbi Kutoka Kwa Migodi Ya Kampuni hiyo.
Mkurugenzi Wa Miradi wa Jamii Katika Kampuni hiyo Pius Kassimu Amesema Jukumu La Kuwalipa Ridhaa Wakaazi Wa Vumbu ni La Kampuni Ya Usagaji Sukari Ya Kiscal, ikizingatiwa kuwa wao ndio waliokodishiwa ardhi ya eneo hilo.
Hata Hivyo Wakaazi Wa Vumbu Wanashikilia Kuwa Kampuni Ya Base Titanium Inafaa Kuwalipa Ridhaa Kutokana Na Kile Wanachodai Kuwa Kampuni Hiyo Imewaletea Madhara Ya Kutosha Kutokana Na Uchimbaji Wa Madini.

Show More

Related Articles