HabariPilipili FmPilipili FM News

Gavana Wa Kaunti Ya Nyeri Wahome Gakuru Afariki

Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru ameripotiwa kufariki  dunia mapema leo asubuhi baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani.

Kulingana na walioshuhudia, ajali hiyo imetokea katika bara bara kuu ya thika- Nairobi eneo la makenji kaunti ya murang’a.

Inaarifiwa gavana Gakuru alikuwa na dereva wake wakielekea nairobi kutoka kaunti ya nyeri wakati wa ajali hiyo. Habari za kifo chake zimetolewa mda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Thika kupokea matibabu.

 

 

Show More

Related Articles