HabariMilele FmSwahili

Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru afariki

Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru amefariki kufuatia ajali mbaya ya bara barani huko kabati kaunti ya Muranga. Gavana Gakuru amefariki akipokea matibabu katika hospitali ya Thika level 5. Baraza la mawaziri wa kaunti hiyo wakiongozwa na Muthui Kariuki wamedhibitisha kifo cha gavana Gakuru. Mwili wa gavana Gakuru unatarajiwa kusafirishwa hadi chumba cha maiti cha Lee hapa Nairobi..

Wakati uo huo viongozi mbali mbali wanaendelea kutuma risala zao kufuatia kifo cha gavana wa Nyeri Wahome Gakuru. Spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi na gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko wameifariji familia ya mwendazake.

Show More

Related Articles