HabariMilele FmSwahili

Wenyeji wa eneo bunge la Kitutu Chache kusini kuchagua mbunge wao leo

Wenyeji wa eneo bunge la Kitutu Chache South Huko Kisii wanamchagua mbunge wao. Idadi ndogo ya wapiga kura imeshuhudiwa asubuhi hii licha ya vituo kufunguliwa mapema kama ilivyoratibiwa. Ni uchaguzi ambao wagombea karibu saba wanamenyana ushindani ukiwa baina ya Anthony Kibagendi wa na Richard Onyonka wa Ford Kenya. Kinyanganyio hiki pia kimewavutia Samuel Omwando wa ODM, Andrew Mokaya wa Wiper, Henry Morara wa KANU na James Kegoro wa PDP. Uchaguzi huu haukuandaliwa Agosti nane kutokana na kifo cha mmoja wa wagombea Leonard Gwaro mwamba. Eneo bunge hili lina wapiga kura 59,017.

Show More

Related Articles