HabariMilele FmSwahili

Mtahiniwa wa KCSE afanyia mtihani katika chumba cha kujifungua kina mama Busia

Mtahiniwa wa KCSE  katika shule ya upili ya St Monica Butunyi iliyoko Butula kaunti ya Busia  amekalia mtihani wake wa  hesabu katika chumba cha kujifungua kina mama.  Hii ni baada yake kuanza kuhisi maumivu ya kujifungua muda mfupi kabla ya kuanza kwa mtihani huo mapema leo. Msimamizi wa hospitali hiyo Dkt Cindy Ekisa anasema  mtahiniwa ataendelea na mtihani wake akiwa hospitalini ili kufanyiwa uchunguzi.

Show More

Related Articles