HabariMilele FmSwahili

Mashirika ya ‘Kura yangu sauti yangu’ na ‘We The People’ yapigwa marufuku ya kuhudumu

Mashirika ya ‘Kura yangu sauti yangu’ na lile la ‘We The People’ yamepigwa marufuku ya kuhudumu mara moja. Afisa mkuu wa bodi ya kudhibiti mashirika Fazul Mohammed ameyashtumu kwa kuajiri wafanyikazi wa kigeni na kuendesha akaunti gushi za benki.

Katika barua, Fazul anasema mashirika hayo kupitia benki za NIC na Citi yamepokea shilingi milioni 36 kutoka kwa ‘George Soros Foundation’ bila kuweka wazi madhumuni ya fedha hizo. Ameyataka mashirika hayo kusitisha shuguli zake mara moja zikiwemo kuingilia masuala ya siasa. Yanajiri hayo saa chache tu baada ya mashirika hayo na lile la Muhuri kujitetea dhidi ya shtuma zinahudumu kinyume cha sheria.

Show More

Related Articles