HabariMilele FmSwahili

Shughuli za uchukuzi zakwama baada ya sehemu ya daraja la Kainuk kuporomoka

Shughuli za uchukuzi zimekwama baada ya sehemu kubwa ya daraja la Kainuk linalounganisha kaunti za Pokot Magharibi na Turkana kuporomoka. Kisa hiki kimejiri kufuatia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko eneo hilo. Katika taarifa mamlaka ya bara bara kuu KENHA imedhibitisha kazi ya ukarabati kwenye bara bara hiyo inaendelea na huenda ikakamilika baada ya siku mbili. Naibu mkurugenzi wa KENHA Charles Njogu amewataka watumiaji bara bara ya Kitale Lokochar Lodwar na Dapal kuwa na subira ukarabati ukiendelea

Show More

Related Articles