HabariPilipili FmPilipili FM News

Hatua ya Nasa Kuwataka Wafuasi wao kususia baadhi ya bidhaa Huenda Ikaathiri Uchumi Wa Taifa

Wafanyibiashara wanaohusika na bidhaa za kampuni ya Safaricom wamekashifu vikali hatua ya viongozi wa NASA kuwataka wafuasi wao kususia bidhaa za kampuni hiyo.

Wakiongea na waandishi wa habari wafanyibiashara hao wamesema hatua hiyo huenda ikaathiri uchumi wa taifa pakubwa.

Kulingana nao hali ya kibiashara imeendelea kushuka tangu msimu wa uchaguzi kuanza huku wakionyesha hofu ya hali kuwa mbaya zaidi iwapo viongozi hawatajiepusha na siasa za mgawanyiko.

Show More

Related Articles