HabariMilele FmSwahili

Peter Wekesa mchezaji wa raga afariki

Siku moja tu baada ya mchezaji wa raga Mike Okombe kuaga dunia , mchezaji mwengine wa raga Peter Wekesa ametangazwa kufariki mapema hii leo.

Peter Wekesa ambaye kwa wakati mmoja aliwai hudumu kama nahodha wa Menegai cream Homeboyz RFC alifariki katika hospitali ya Mariakani kule Mombasa baada ya kuhusika katika ajali hapo jana akiwa na pacha wake John Wekesa.

Wawili hao waliaga dunia wote. Itakumbuka kwamba mwezi Januari mwaka huu walimpoteza kaka yao mkubwa Andrew Wekesa ambaye pia alikuwa mchezaji wa raga. Andrew wekesa aliuwawa na watu wasiojulikana katika maeneo ya Kitengela.

Show More

Related Articles