HabariPilipili FmPilipili FM News

Hassan Abdi: Hatutafika Mbele Ya Bodi Ya Kudhibiti Utendakazi Wa Mashirika Ya Kijamii

Mkurugenzi wa shirika la Kijamii la MUHURI Hassan Abdi Abdle, amedokeza kuwa hawatafika mbele ya bodi ya kudhibiti utendakazi wa mashirika ya kijamii Nchini  kama ilivyoagizwa, ili kujibu madai  kwamba wana njama ya kuwasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Mteule Uhuru Kenyatta.

Hassan  amesema  madai hayo yanakosa msingi na ambayo  yanalenga  kudhalilisha utendakazi wa mashirika ya Kijamii nchini

Shirika hilo na lile la Inuka Kenya pamoja na Katiba Institute, yanadaiwa kushirikiana na shirika la kijamii la Kura Yangu Sauti Yangu ili kuwasilisha kesi katika mahakama ya juu Nchini, kwa lengo la Kupinga ushidi wa Rais Kenyatta.

Show More

Related Articles