HabariMilele FmSwahili

Watu wawili wafariki kutokana na mafuriko Marsabit

Watu wawili wamedhibitishwa kufariki huku wengine wawili wakiwa hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko  katika eneo la Olom eneo bunge la Horr Kaskazini kaunti ya Marsabit. Kulingana na mwakilishi wadi ya Maikona Buke Diba, wawili hao mume na mkewe walisombwa na maji kufuatia mvua ambayo pia imeziacha  zaidi ya familia 72 bila makao. Aidha anasema imekuwa vigumu kuwafikishia misaada waathirika kutokana na kuharibiwa kwa barabara.

Show More

Related Articles