HabariMilele FmSwahili

Mgomo wa waadhiri wa vyuo vikuu waingia siku ya sita leo

Mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu unaingia siku ya sita hii leo huku wanafunzi wa vyuo vikuu wakitishia kususia chakula kuanzia siku ya jumatano kulalamikia mgomo huo. Mwenyekiti wa UASU Muga  Kolale na katibu Constatine Wesonga wameshikilia msimamo kuwa wanachama wao hawatarejea kazini hadi pale serikali itakapotoa shilingi bilioni 5.2 zilizodhibitishwa na bunge kutekeleza mkataba wao wa mwaka wa 2013- 2017. Wamekanusha madai kuwa mgomo wao umechochewa kisiasa. Nao wanafunzi wa vyuo  tofauti wakiongozwa na Edwin Kegoli wanasema wanaathirika zaidi na ukosefu wa wahadhiri darasani.

Show More

Related Articles