HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

NASA imewataka wafuasi wao kususia bidhaa za kampuni tatu

Msukumo wa upande wa upinzani NASA wa kutaka wafuasi wao kususia baadhi ya bidhaa na huduma kutoka kwenye kampuni ambazo NASA inadai kuwa zina uhusiana mkubwa na serikali ya Jubilee unazidi kusua hisia mseto nchini.

Aidha msukumo wa maajuzi wa eneo la Pwani kutaka kujitenga pia umeonekana kuyumbisha mkondo wa mambo nchini.

Viongozi wa Jubilee wanadai kuwa njama ya NASA ya kulemaza uongozi wa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto haitafaulu huku wakizidi kuwataka wakenya kuwa watulivu na kujiepusha na ghasia wala tofauti za kidini, kisiasa na kikabila.

Je, msukumo wa NASA ni wa nia njema au ni njama fiche? Anders Ihachi anafafanua zaidi.

Show More

Related Articles