K24 TvNEWSSwahiliVideos

Shinikizo la NASA : Maelfu ya wakenya huenda wakapoteza ajira endapo litatekelezwa

Huenda wakenya kati ya elfu sabini na elfu mia moja wakapoteza ajira  humu nchini, iwapo amri ya muungano NASA kwa wafuasi wakenya kususia bidhaa kutoka kwa kampuni kadhaa itatekelezwa.
Haya yamesemwa na katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli, ambaye ameutaka muungano huo wa upinzani kutafuta njia mbadala za kushinikiza ajenda zao, badala ya kutishia kususia za bidhaa.
Atwoli ameyasema haya huku NASA ikisema kuwa tangazo lake kwa wafuasi kususia bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni za Safaricom, Brookside na Bidco limeanza kutekelezwa na kuzaa matunda.

Show More

Related Articles