HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi wa vyuo vikuu watishia kuandamana kulalamikia mgomo wa waadhiri unaoendelea

Wanafunzi wa vyuo vikuu wametishia kushiriki maandamano kulalamikia mgomo unaoendelea wa wahadhiri .Kupitia viongozi wao wanafunzi hao wanasema mgomo huo umeathiri masomo na kuitaka serikali kushughulikia lalama zilizowasilishwa na wahadhiri ili kuhakikisha masomo yanaendelea. Wanasema watashirikiana na vyuo vikuu vya kibinafsi kuandamana katikati mwa jiji kuwasilisha lalama zao. Wahadhiri wa vyuo vikuu walianza rasmi mgomo mapema juma hili kuishinikiza serikali kutekeleza mkataba waliofikiwa wa kuwapa nyongeza ya mshahara.

Show More

Related Articles