HabariMilele FmSwahili

Mailu aagiza kusitishwa kwa agizo la usimamizi wa bima ya NHIF

Waziri wa afya Cleopa Mailu ameagiza kusitishwa mara moja kwa agizo la usimamizi wa hazina ya bima NHIF kuwataka wakenya wanaotumia huduma  ya NHIF kupokea huduma za  kutibiwa na kuruhusiwa kuondoka  kupata huduma hizo mara 4 pekee kwa mwaka. Waziri Mailu anasema agizo hilo litasitishwa ili kutoa  nafasi kwa majadiliano zaidi kati ya  bodi ya NHIF na  wadau wengine. Amewataka wateja wanaotumia huduma hiyo kuendelea kutibiwa jinsi ilivyokuwa hapo awali.

Show More

Related Articles