HabariMilele FmSwahili

Nyongo alalamikia uagizaji wa sukari kutoka nje

Gavana wa Kisumu Anyang Nyongo amelalamikia uagizaji wa sukari kutoka nje, akisema hatua hiyo imeathiri bei ya sukari ya humu nchini. Akiongea alipozuru kiwanda cha Chemelil, anasema licha ya umuhimu wake, serikali haijachukua hatua za kutosha kuboresha sekta ya sukari nchini. Mwenzake wa Nandi Stephen Sang kwa upande wake amesisitiza haja ya juhudi za pamoja kushughulikia matatizo yanayokabili sekta hiyo. Waziri wa kilimo Willy Bett hata hivyo ametetea hatua hiyo akisema ilitokana na kiangazi cha muda mrefu kilichotatiza uzalishaji wa miwa.

Show More

Related Articles