HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Wauguzi warudi kazini kuhudumia wagonjwa kwenye taasisi za umma

Siku moja baada ya mgomo wa wauguzi uliodumu kwa takriban miezi mitano wauguzi kote nchini wameonekana kurejea kazini.

Katika hospitali nyingi nchini wauguzi  hii leo walirudi kazini na kurejelea kutoa huduma za matibabu, huku wagonjwa wengi wakisema kusitishwa kwa mgomo huo kutawasaidia sana kwani wengi wao walihangaika wakitafuta matibabu kwa kukosa fedha za kulipia hospitali za kibinafsi.

Wauguzi wengi pia wanakiri kuwa makubaliano waliyofanya jana  na baraza la magavana pamoja na serikali kuu yamewapa motisha wa kufanya kazi kwani wana imani mahitaji yao sasa yatashugulikiwa.

Show More

Related Articles