HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwadeghu Akanusha Kusambaza Jumbe Za Chuki Taita.

Aliyekuwa Mbunge wa Wundanyi, Thomas Mwadeghu amekana kuhusika na jumbe zinazosambazwa katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Taita Taveta pamoja na mitandao ya kijamii, kumtishia Gavana wa Kaunti ya Taita Taveta, Granton Samboja.

Mwadeghu amesema wanaosambaza jumbe hizo wana njama ya kumharibia jina, na kuitaka idara ya polisi kufanya uchunguzi wa haraka ili kuwachukulia hatua kali wahusika.

Kwa upande wake gavana wa Taita taveta Granton Samboja ameyataja matamshi hayo kama kelele za chura, akisema ajenda yake kuu ni kufanikisha maendeleo katika kaunti hiyo.

Show More

Related Articles