HabariPilipili FmPilipili FM News

Wauguzi Mombasa Waomba Radhi Wakaazi Kwa Kuhangaika Wakati Walipo Goma.

Wauguzi katika hospitali kuu kanda wa Pwani wameomba wakaazi wa Mombasa msahaha kwa mahangaiko waliopata wakati walipokuwa kwenye mgomo uliodumu siku 150.

Katibu mkuu wa muungano wa Wauguzi, kaunti ya Mombasa Peter Maroko amewaomba wauguzi waliorejea kazini leo kutowadhalilisha wenzao ambao walikuwa wamerejea kazini wakati mgomo ukiendelea.

Wakati uo huo wangonjwa katika hospitali hiyo wamefurahia  hatua ya wauguzi kurejea kazini, huku wakionyesha matumaini ya kupata huduma muhimu za afya.

Hapo jana chama cha wauguzi kilitia saini mkataba wa maelewano kati yake na baraza la magavana nchini, katika hali ambayo mkataba huo unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha siku 30.

Show More

Related Articles