HabariMilele FmSwahili

NASA yatoa orodha ya bidhaa ambazo wafuasi wake wahitajika kususia

Muungano wa NASA sasa umetoa orodha ya bidhaa ambazo wafuasi wake watahitajika kususia. Kwenye taarifa iliyosomwa na wanasiasa tofauti wa NASA, wanasema wamechukua hatua hiyo kwa kile wanadai kampuni zinazotengeneza bidhaa hizo zinahusiana na serikali. Wanasema hatua hiyo itatumika kama moja wapo ya shinikizo kuleta mageuzi nchini. Huku wakitoa makataa ya wiki moja, wanasiasa hao wanawataka wafuasi wao kutumia bidhaa za kampuni mbadala. Japo hawajaelezea bayana iwapo pia watasusia sarafu za taifa zilizo na picha ya rais mwanzilishi wa taifa, wanasema picha hiyo inafaa kuondolewa kwa madai sheria iliagiza hivyo.

Show More

Related Articles