HabariMilele FmSwahili

KNHCR: Watu 54 ndio waliofariki kati ya Agosti na Oktoba wakati wa uchaguzi

Watu 54 ndio waliofariki kati ya Agosti na Oktoba wakati wa kipindi cha uchaguzi. Haya ni kwa mujibu wa tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu nchini. Tume hiyo inasema watu wengine 150 wakiwemo watoto na polisi walijeruhiwa. Watano kati ya waliofariki, waliuwawa wakati wa kipindi cha mwarudio ya uchaguzi 4 wakifariki kaunti ya siaya na 1 kisumu. Mwenyekiti Kagwiria Mbogori anasema maeneo mengi yaliyoshuhudia ghasia ni ngome za NASA wakidai polisi walitumia nguvu kupita kiasi kuwakabili wafuasi wa NASA. Ni takwimu zinazotolewa huku idara ya polisi ikipinga takwimu zinaotolewa na mashirika hasa ya kijamii nchini.

Show More

Related Articles