HabariMilele FmSwahili

Jamii kwenye mpaka wa Kisumu, Nandi na Kericho zaafikiana kukomesha uhasama baina yao

Jamii zinazoishi mpakani mwa kaunti za Kisumu, Nandi na Kericho zimeafikiana kukomesha uhasama wao na kuishi kwa amani. Wenyeji hao wamebaini kuwa uhasama wa kila mara baina yao umekwamisha maendeleo na kuzua chuki hivyo unafaa kukomeshwa.
Magavana Stephen Sang na Anyang Nyongo nao wameahidi kufanya kila wawezalo kuhakikisha amani ya kudumu mpakani humo. Wakihutubu kwenye msafara wa amani, magavana hao aidha wamewataka polisi kuwakabili wahalifu wanaotumia fursa hiyo kuwahangaisha wenyeji wasio na hatia.

Show More

Related Articles