HabariMilele FmSwahili

Makundi ya kidini yaendelea kukosoa wito wa kubuniwa wadhifa wa waziri mkuu

Makundi ya kidini yameendelea kukosoa wito wa baraza la makanisa nchini NCCK kubiniwa wadhifa wa waziri mkuu ili kusuluhisha mgogoro wa kisiasa nchini. Kulingana na mwenyekiti wa baraza wa wahubiri wa kiislamu kanda ya North Rift Abubakar Bini viongozi wa kidini nchini wamefeli kutoa mwongozo usioegemea upande wowote wa kisiasa. Kauli sawa imetolewa na viongozi wa makanisa kutoka Thika na Kiambu ambao pia wameusuta muungano wa NASA kwa kuanzisha vuguvugu la uasi NRM.

Show More

Related Articles