HabariMilele FmSwahili

Huduma za matibabu zatarajiwa kurejea kama kawaida kuanzia leo

Huduma za matibabu zinatarajwia kurejelewa kama kawaida kuanzia leo, wauguzi wakirudi kazini baada mgomo wa zaidi ya siku 150 kusitishwa. Waziri wa afya Dkt Cleopa Mailu amewataka wakenya kuanza kufika katika hospitali za umma kutafuta huduma akiahidi kuwa mashauriano yataendelea kuona kwamba sekta ya afya haiathiriki tena na mgomo. Wakati huo huo mwenyekiti wa masuala ya afya katika baraza la magavana gavana James Ongwae naye anasema watahakikisha kama magavana huduma za afya zinaendelea kuimarishwa zaidi ili kuwafikia wakenya wote.

Show More

Related Articles