HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahadhiri Wa TUM Waanza Mgomo.

Wahadhiri wa chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa TUM wameanza rasmi mgomo wao hii leo kuishinikiza serikali kuwapa nyongeza yao ya mishahara.

Joseph Ngare ambaye ni mwenyekiti wa  muungano wa wahadhiri katika chuo hicho, anasema wameafikia uamuzi huo baada ya serikali kushindwa kutekeleza mkataba wa malipo yao kama ilivyoagizwa na mahakama ya viwanda nchini.

Kulingana nao mshahara wanaopata ni duni ikilinganishwa na mchango wao kwa jamii.

Ngare amesema jukumu sasa la kufundisha wanafunzi limeachiwa utawala wa chuo hicho kwa sasa hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa.

Kwa sasa wahadhiri kutoka vyuo vikuu 28 vya umma wanaendelea na maandamano kushinikiza kutekeleza kwa matakwa yao.

Katibu wa muungano wa UASU Constatine Wasonga ameilamu serikali akisema imekuwa ikiwahadaa na kushikilia hawatarejea kazini hadi shilingi bilioni 5.2 za kufanikisha mkataba huo zitakapotolewa.

Show More

Related Articles