HabariPilipili FmPilipili FM News

Mvua Yatatiza KCPE Kwale.

Shughuli za kukamilisha mtihani wa kitaifa wa darasa la nane  KCPE kwa takriban shule 26 katika kaunti ya Kwale zimetatizika pakubwa hii leo kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo la Pwani.

Hii ni kutokana na baadhi ya barabara kufurika maji na kukatika katika sehemu tofauti hali iliyotatiza usafirishaji wa mitihani na pia kuchangia watahiniwa kukosa kufika shuleni kwa wakati ufaao.

Kaimu kamishna kaunti ya Kwale Mwangi Kahiro amethibitisha  tatizo hilo akisema kuwa kufikia mwendo wa saa tano  watahiniwa wa shule zilizoathiriwa na mvua ,walikuwa bado hawajaanza mtihani wao wa mwisho.

kati ya walioathiriwa ni Watahiniwa  kutoka shule 22 eneo bunge la kinango pamoja na watahiniwa wa shule 4 eneo bunge la matuga.

Show More

Related Articles